Saturday, 5 November 2016

TAARIFA KWA MAMENEJA WA KANDA

TAARIFA KWA MAMENEJA WA KANDA
18/10/2016
Mnajulishwa kwamba Kitengo chetu cha Habari na Mawasiliano kipo katika maandalizi ya Toleo Na. 04 la Jarida la OSHA. Ili kuhakikisha kwamba Jarida letu linakuwa jumuishi na linasheheni habari kutoka katika kanda zote, mnaombwa kuandika Habari na Makala mbali mbali kutoka katika kanda zenu.
Maudhui ya habari hizo yajikite katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka huu na kila habari iandikwe katika lugha zote mbili (Kiswahili na Kingereza). Kwa ufafanuzi zaidi mnaweza kuwasiliana na kitengo husika.
Mwisho wa kuwasilisha habari hizo ni Octoba 31, 2016 na zitumwe katika eleuterm@gmail.com au gyunaa@gmail.com
Nawatakia utekelezaji mwema.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.